Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mngereza: Maadili ni sifa kwa wasanii kitaifa

3f81199a41c3946ee5bb2f212e778bf4 Mngereza: Maadili ni sifa kwa wasanii kitaifa

Fri, 25 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema maadili ni moja ya sababu ya wasanii kuchaguliwa katika shughuli za kitaifa.

Akizungumzia Dar es Salaam jana Mngereza alisema wapo baadhi ya wasanii wa kike ambao wanafanya kazi zao vizuri na kufuata maadili ndio maana wanachaguliwa katika shughuli za kitaifa.

"Wapo wasanii wengi wa kike ambao wanafanya vizuri kazi zao na kufuata maadili bila kumtaja mmoja mmoja na hao ndio wanaochaguliwa katika shughuli za kitaifa na wasiofuata maadili pia wanajielewa, nawaomba wajirekebishe,"alisema.

Pia alisema "Kanuni zinazotolewa na BASATA ni kanuni za Bunge za mwaka 2018 sheria no: 23 za mwaka 1979 ambazo zinatoa maelekezo ya kuzingatia.

Aidha msanii kabla ya kutoa wimbo anatakiwa kuhakiki kabla ya kufika kwa msikilizaji na mtazamaji.

Chanzo: habarileo.co.tz