Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlimbwende amfungulia P. Diddy kesi nyingine ya udhalilishaji

P Diddy X Mc Mlimbwende amfungulia P. Diddy kesi nyingine ya udhalilishaji

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani #Diddy anakabiliwa na kesi nyingine ya unyanyasaji wa kingono ambayo imefunguliwa hivi karibuni na mwanamitindo wa zamani Crystal McKinney, tukio linalodaiwa kutokea 2003 huko New York City.

Kwa mujibu wa tmz imeeleza kuwa Mc Kinney alipokuwa na miaka 22 alialikwa kwenye hafla ya wiki ya mitindo ya wanaume huko Cipriani Downtown ambapo alikutana na Combs, wakati wa sherehe mwanadada huyo alikwenda bafuni na kudai kuwa #Diddy alimfuata chooni na kumlazimisha kufanya ngono ya mdomo.

Aidha katika maelezo ya mwanamitindo huyo aliendelea kwa kudai kuwa rapa huyo alitumia nguvu mpaka kupelea kuzimia, ambapo baada ya kurejesha fahamu alingundua kuwa alishambuliwa kingono.

Hata hivyo, kesi hiyo haijaweka wazi kama ni yamadai ya kulazimishwa kufanya ngono ya mdomo au kushambuliwa kingono alipokuwa amepoteza fahamu.

#CrystalMcKinney amedai kuwa kufuatia na tukio hilo alipata msongo wa mawazo na kutaka kujiua kwa zaidi ya mwaka hivyo amefungua kesi hiyo kutaka kulipwa fidia ya udhalilishaji huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live