Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkubwa Fella afunguka Wasafi kutokwenda kumzika Haitham

Fella Haitham Mkubwa Fella afunguka Wasafi kutokwenda kumzika Haitham

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aitwaye Mubwa Fella amekiri kuwa Wasafi hawakwenda kwenye mazishi ya msanii mwenzao, Haitham Ghazal Seif 'Haitham Kim' ambaye alifariki hivi karibuni na kuzikwa kwatika makaburi ya Kisutu.

Mkubwa Fella amejibu hayo wakati akihojiwa na vyombo vya habari Ruangwa mkoani Lindi ambapo timu nzima ya Wasafi na wasanii wa WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz ilikwenda kwa ajili ya Tamasha la Wasafi Festival huku akiongeza kuwa wamepanga kufanya kitu kikubwa kwa familia ya marehemu Haitham.

"Ni kweli hatukuhudhulia mazishi ya Haitham Kim lakini hiyo haimaanishi hatujashiriki, kushiriki msiba siyo tu kwenda makaburini kuzika wala kwenda kukaa nyumbani kwa Marehemu.

"Sisi kama Wasafi hatukuonekana msibani lakini tuna mpango wa kuifanyia kitu famil ia ya marehemu Haitham Kim," amesema Mkubwa Fella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live