Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkubwa Fella: Hakuna atakayeweza kutuzidi labda tufe

Fellaa2 Mkubwa Fella: Hakuna atakayeweza kutuzidi labda tufe

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Said Fella ametamba kwamba, kutokana na uthubutu wao, hakuna lebo nyingine ya muziki Bongo inayeweza kuwafunika labda itokee wao wamefariki au wameamua kuachana na kazi hiyo.

Fella amesema, silaha kubwa ya mafanikio yao ipo kwenye kuthubutu kuweka fedha nyingi kisha kusubiri matokeo ya kupata nyingi zaidi baada ya muda fulani.

“Kuna msanii unadhani anaweza kuweka milioni 200 kwa ajili ya video moja halafu asubiri? Sisi tuliweza kuthubutu hata kama hatukuwa na hela ya kula lakini tuliona ni bora kuwekeza fedha nyingi na kusubiri matokeo na kweli tulifanikiwa,” alisema Fella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live