Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkubwa Fella: Alichozungumza P Funk ni pumba

Fella P Funks Mkubwa Fella na P Funk

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmmoja wa mameneza wa Lebo ya WCB, Mkubwa Fella amemjibu producer mkongwe wa muziki Bongo, P Funk ‘Majani’ kufuatia kauli yake ya kwamba, lebo hiyo inawanyonya na kuwakandamiza wasanii wake.

Fella amesema ameshangazwa na kauli ya mkongwe huyo na kudai mikataba ya WCB msanii anachukua asilimia 40 na uongozi unachukua asilimia 60 kwa kuwa WCB inafanya kazi kubwa ya kusaidia msanii husika kukua ikiwemo maandalizi ya video na usambazaji wa kazi zake za muziki.

“Angesema mwendawazimu ningesema ana haki ya kuzungumza, lakini alivyozungumza Majani naona kama anakosea, sababu anaujua huu muziki na tasnia nzima, yeye kama mkongwe naona kama alifeli.

“Nusu ya sanaa yangu nadhani tulisaidiana pale kwake, sababu wakati huo namsimamia Juma (msanii Juma) na yeye anamsimamia Juma (msanii Juma Nature), kwa hiyo nimesikiliza lakini nimepuuza kwa sabanu naona huyu mbona ana akili lakini leo kazungumza tofauti.

“Sijui wakati anazungumza kuna vitu alikuwa ametumia kabla? Kuna ulevi labda alitumia kabla? Lakini kidhati kabisa alichozungumza ni pumba.

“Tukizungumzia Daz Nundaz, Ferouz, Juma Nature, Profesa Jay na wengine wengi, wao wasanii wana malalamiko mengi kwake.

“Tunamuona kama kaka, namuona kama mdogo wangu, yeye angekuja tukazungumza naye akafahamu, hata anapozungumza na vyombo vya habari anasimama katika njia moja kuliko kulumbana.

“Hatukatazi msanii kutoka WCB, lakini tunataka afuate utaratibu. Ulivyokuja si umesaidiwa, na umefika sehemu nzuri? Wewe sema jamani ndugu zangu tumalizane kama alivyofanya Rayvanny.

“Unazungumza huku, halafu kwenye makaratasi kuko sahihi, ma’ke mmalizane. Sasa hivi wanamshambulia Diamond kwamba kafanya mambo mabaya, hawasemi kwamba Diamond kafanya mambo mazuri, kumtoa alipotokea Rayvanny.

“Rayvanny alikuwa ‘Mkubwa na Wanae’ anajifunza tu, lakini huku ndiko kwenye hela, kaanza kupata pesa, mseme basi kwamba Diamond kafanya hivi.

“Nachojua kuna asilimia 40 na asilimia 60, na hii asilimia 60 kuna mameneja humo humo, mkurugenzi humo humo, lakini pia kuna yeye kufanyiwa video, kurekodiwa, ndio hivyo vinavyofanyika, wewe ukipewa asilimia 40 katumie na ndugu zako, lakini hii asilimia 60 bado kuna vitu vya kuendeleza muziki wako.

“Unajua mtu akiporomoka kiuchumi ndipo anakwenda kuropoka ropoka vitu tofauti, tukienda hivyo tasnia haiwezi kukua, itakuwa ujinga tu. WCB hatukutegemea kama mtu mkubwa kwenye tasnia atazungumza hayo,” amesema Fella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live