Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkojani, JB watakata tuzo za filamu

Images (29) Jb.jpeg Mkojani, JB watakata tuzo za filamu

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye tuzo za filamu mwaka 2022 zimefikia ukingo ambapo kwa upande wa wasanii wa kiume bora Nkwabi Ng'wanamala maarufu kwa jina la Mzee Kikala wa tamthiliya ya Kombolela ameibuka mshindi.

Sambamba na hilo kwa upande wa msanii bora wa kike,Tunu Mbegu wa filamu ya 'Still Ok to Date' ameibuka kidedea.

Tuzo hizo ambazo hii ni mara yake ya pili kutolewa tangu kuanzishww kwake, zimetolewa usiku wa jana jijini Arusha ambapo wasanii  169  walikuwa wakichuana na filamu 39 zilikuwa zikishindanishwa.

Katika kinyang'anyiro hicho waliokuwa wakichuana katika kipengele cha msanii bora wa kiume   alikuwepo Saam Nawanda  na Ayoub Bombwe na Mzee Kikala wa tamthiliya ya Kombolela ambaye ndio ameibuka mshindi.

Wakati kwa upande wa msanii bora wa kike Tunu ambaye kawa mshindi  alikuwa anachuana na wasanii Wema Sepetu,Bi Star,Irene Paul, Thecla Mjata, Nyota Waziri .

Wengine walioshinda katika tuzo hizo ni mchekeshaji  Mkojani ambaye ameng'ara kwenye kipengele cha mchekeshaji bora.

Mkojani alikuwa akipambambanishwa na Lucas Mhavile 'Joti',  Tabu Mtingita, Andrew Ngonyani (Brother K) aliyepata umaarufu kupitia vichekesho vya Futuhi.

Wengine ni Gladness Kifaluka wa vichekesho vya Kitimtim na Ally Chuma wa vichekesho vya "Jambo na Vijambo".

Aidha upande wa muongozaji bora,Leah Mwendamseke maarufu 'Lamata' aliondoka na ushindi.

Lamata ambaye ni muongozaji wa filamu ya Jua Kali, alikuwa akishindanishwa na waongozaji wengine akiwemo Neema Ndempaya, Honeymoon Aljabri, Leah  Mwendamseke, Florence Mkinga na Christina Pande.

Aidha msanii Jacob Steven'JB' alitangazwa kuwa mshindi katika kipengele cha  chaguo la watazamaji kipengele kilichukuwa kinashindaniwa na wasanii 19.

 Pia katika usiku huo wa tuzo,filamu ya Vuta 'Nkuvute iliyotajwa katika vipengele 13 imechujua ushindi katika kipengele cha Best Producton Design,Best Screen Play na Best Set Design.

Filamu hiyo ndio imepekewa kushindanishwa katika tuzo za kimataifa za Oscar mwaka huu zitakazotolewa nchini Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live