Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mkia wa ng'ombe ulivyomnyima kijnana mke

BORAA Md Mkia wa ng'ombe ulivyomnyima kijnana mke

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii ni hadithi ya kijana ambaye alitamani kuoa binti mzuri wa mkulima, Binti ambaye alikuwa ni mrembo kuwahi kumshuhudia katika upeo wa macho yake. Alikwenda kwa mkulima kuomba ruhusa yake na kumuambia juu ya hitaji lake la kumuoa binti yake.

Mkulima akamtazama na kujibu, “Mwanangu, nenda usimame kwenye shamba hilo ambalo unaliona kisha nami nitawaachilia mafahali watatu, mmoja mmoja. Ukiweza kukamata mkia wa fahali mmoja kati ya wale ng’ombe watatu, unaweza kumwoa binti yangu.”

Kijana akabubali na alisimama kwenye malisho akimngoja fahali wa kwanza. Mlango wa zizi ulifunguliwa na kutoka nje fahali mkubwa zaidi, mwenye sura mbaya zaidi ambaye hajawahi kuona kabla na akiogopesha.

Aliamua kwamba fahali mmoja atakayefuata atakuwa chaguo bora kuliko huyu, kwa hiyo alikimbia kando na kumwacha fahali huyo apite kwenye malisho nje ya lango ama zizi.

Mlango wa zizi ukafunguliwa tena. Ajabu hakuwahi kuona kitu kikubwa kama hicho,n'gombe alionekana mkubwa na mkali akiwa na pembe zilizo chongoka . kijana aliguna kuona fahali huyo akimtazama .

Vyovyote vile fahali aliyefuata atakuwa chaguo bora kuliko hawa waliopita, Alikimbilia kwenye uzio na kumwacha fahali apite kwenye malisho, nje ya lango la zizini.

Mlango ukafunguliwa mara ya tatu, Tabasamu likamjia usoni. Alietoka fahali mdogo sana na dhaifu, kijana akajisemea "Hakika huyu ndiye ng'ombe dume mdogo aliye dhaifu zaidi kumshuhudia.

Fahali huyo alipokuja mbio, alijiweka sawa na kujitayarisha kuruka kukamata mkia wake, alimrukia lakini hakuambulia kitu maana fahali huyo hakuwa na mkia!.

Hivyo kijana akawa ameshindwa kufaulilu mtihani aliopewa, Funzo Maisha yamejawa na fursa nyingi, zipo rahisi na ngumu. Mara utakapojaribu kuacha fursa ikupite haitojirudia tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live