Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya anayefanana na Mbosso ataka vipimo vya DNA

Mbosso Ms(2) Mkenya anayefanana na Mbosso ataka vipimo vya DNA

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, kumekuwa na msanii mmoja kutoka chini Kenya ambaye amekuwa akidai kwamba Mbosso ni baba yake.

Msanii huyo chipukizi kwa jina Demmah B ambaye anafanana na Mbosso kwa karibia kila kitu amekuwa akishiriki mahojiano na waandishi wa habari za mitandaoni akisema kwamba hashangai kufanana na msanii wa WCB Wasafi kwani anamfahamu kama baba yake licha ya kuwa hawajawahi kutana hata siku moja.

Msanii huyo sasa amefikia hatua nyingine kwa kudai kwamba anachotaka ni vipimo vya DNA ili kuthibitisha ukweli wake ambao amekuwa akiushikilia kwa muda mrefu.

Demmah B alisema kwamba Mbosso ni baba yake aliyemtelekeza na sasa anateseka huku hali ya kuwa baba yake anapunja maisha mazuri nchini Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live