Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili na mtayarishaji wa muziki nchini Kenya, Wiliam Getumbe amefunguka kuhusu hali ya kuwa mtu wa kukojoa kitandani na jinsi anavyoishi na hali hiyo.
Getumbe amesema mkewe, Virginia Masitha, anafahamu hali yake na ndiye anayemsaidia kumvalisha nepi kila usiku kabla ya kwenda kulala, ili kuepuka kulowesha godoro.
Alidai kuwa watu wazima wengi hulowesha vitanda vyao usiku, lakini wanaona aibu kuwaeleza wapenzi wao, jambo ambalo anadai limevunja nyumba nyingi.
Alimpongeza mkewe kwa kumvumilia na hata kumbadilisha nepi kila usiku.
“Familia nyingi zimevunjika kwa sababu ya kukojoa kitandani. Hata hivyo, mke wangu ananielewa sana, kila usiku ananivalisha nepi bila kunidharau.
Wanaume wengi wanatumia pampers, haswa wanafunzi wa shule za sekondari, walevi, na wale ambao ni wagonjwa mahututi. Nashauri wanaume wasiogope kutumia nepi; ndiyo njia pekee ya kuweka chumba cha kulala kuwa safi,” alisema.