Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wangu alinisaidia kuacha madawa ya kulevya - Mr Blue

Mke Wangu Alinisaidia Kuacha Madawa Ya Kulevya   Mr Blue Mke wangu alinisaidia kuacha madawa ya kulevya - Mr Blue

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki Blue Byser amefunguka kuhusiana na safari yake ya maisha na Muziki huku akisema kuwa kipindi anaanza muziki walitokea watu ambao ndio ilikuwa chanzo cha yeye kudondoka kimuziki kutokana na starehe.

Akifanya mahojiano na kituo cha Habari cha BBC, Mr Blue amefunguka kuwa familia ndio chanzo kikubwa yeye kurudi kwenye ramani kwani aligundua kuwa ameshaingia kwenye majukumu ya kifamilia.

“Mimi mke wangu namshukuru sana kwani yeye ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kubadilika, Alikuwa ananiambia taratibu vitu vya kufanya na badae aliposhika ujauzito ndio nikagundua naenda kuwa na familia.

“Mimi wakati naanza muziki nilikuwa mtoto na sikuwa na rafiki lakini watu walikuja wakijifanya wananijua wamesoma na mimi kwahiyo ule ushkaji mtu akichoma na mimi nachoma mara pombe nikawa siendi studio, Mimi nimeharibiwa na watu waliokuja baada ya mimi kuwa Staa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live