Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Ricardo Momo amchana Juma Lokole

Gfb Juma Lokole Df Mke wa Ricardo Momo amchana Juma Lokole

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mke wa Ricardo Momo, Malaika Cute ameamua kuvunja ukimya na kumchana mdaku Juma Lokole akidai kuwa amekuwa akimsema kila siku kwa mabaya.

Malaika Cute amedai kuwa Lokole anatumika kumchafua jambo ambalo hatofanikiwa kamwe huku akimtaka kuachana na maisha yake kwani hayamhusu.

“Binadamu wote ni sawa, tofauti yetu inakuja tu pale kwenye uhalisia wetu. Mimi nina mapungufu mengi tu kama binadamu, kwa maana aliyekamilika ni Mungu pekee yake.

“Lakini unatokea unaniandama kila ukiamka ni mimi, chuki uliyonayo wewe ni ya nini na ukiulizwa tunagombea nini unalo la kujibu?

“Mimi nitabaki kuwa mimi hata ufanye nini huwezi nishusha na unalotaka pia halitokuawa kwa maana mpaka hapa ni Mungu tu.

“Uchawa una mwisho na uchawa ufanye kama wengine unaweza msifia bosi wako bila kuponda wengine.

“Nakuangalia nikisema nikuwazie nashindwa maana hata sikuelewi una jinsia gani ya kike au ya kiume. Maana kiuhalisia ni mwanamme lakini maisha yako ongea yako kila kitu chako ni dada sikitu.

“Utahangaika sana na mimi, kashindwa bosi wako utakuwa wewe mbwa usokuwa na geti? Niache na sina muda na shobo zako, unasujudia binadamu wenzio hata mungu humuogopi.

“Unayako kibao unaweza kuyasema kwa page yako kila siku na watu mbona ya shoga yako anayo mengi tena machafu na yakusikitisha? Mbona huyasemi au kwa sababu ni bosi wako? Basi mwambie bosi wako aongezee dau maana unajitaidi sana,” amesema Malaika Cute.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live