Kama ilivyo kawaida kwa wanandoa hawa KanyeWest na Bianca Censori kuvaa mavazi ya kushangaza katika jamii, hivi karibuni mke wa Kanye amezua taharuki kwa watu nchini Italy baada ya kuvaa vazi lenye kuonesha utupu wake.
Bianca alionekana akiwa katika vazi ambalo limetafsiriwa kama ukosefu wa maadili kwenye jamii ambalo limekuwa likimuonesha mtupu huku akikatiza mitaani.
Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ imeripoti kuwa, raia wa maeneo aliyopita Bianca walishangazwa na uvaaji huo na kushindwa kuvumilia hadi kutoa taarifa polisi kwa kuripoti juu ya vitendo hivyo ambavyo kwa mujibu wa sheria za Italy hupelekea kutozwa faini ya zaidi ya TSh 25 milioni au kifungo cha miaka 4.