Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa John Legend afunguka "mimba yangu haikuharibika, ilitolewa"

FB IMG 1663387219250 John Legend na mkewe

Sat, 17 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwana mitindo wa Marekani Chrissy Teigen amefunguka kuhusu tukio la huzuni ambalo lilimtokea miaka miwili iliyopita ambapo alimpoteza mtoto wake (Jack) ambaye hakuwa amezaliwa, amesema alimpoteza kutokana na kutolewa kwa ujauzito (abortion) na sio kuharibika mimba (miscarriage) kama ambavyo ilielezwa.

Kwenye mahojiano yake mapya, Teigen mwenye umri wa miaka 36 akiwa na watoto wawili huku akitegemea mwingine kwa sasa na mumewe John Legend, amesema alishtuka kugundua kwamba alifanyiwa ‘abortion’ ili kunusuru maisha yake kwa mtoto ambaye hakuwa na nafasi tena ya kuishi.

Anasema ilibidi asizungumze ukweli kutokana na jamii kuona kitendo hicho ni cha ajabu na kischokubalika, hivyo ikabidi adanganye kwa kusema ujauzito ule uliharibika yaani miscarriage.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live