Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mke hatakiwi kujua 'password' na mume wake

PASSWORD Mke hatakiwi kujua 'password' na mume wake

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Mawasiliano TCRA, Robin Ulikaye amesema kuwa si vizuri mke au mume kujua password ya mwenza wake ambayo ameweka kwenye kifaa chake anachotumia kwa ajili ya mawasiliano.

Ulikaye amesema hayo kufuatia wimbi kubwa la ndoa nyingi kuvunjika na hata wengine kutoana uhai kwa sababu ya wivu wa mapenzi huku baadhi yao wakihisi kusalitiwa katika mahusiano yao na chanzo kikitajwa kuwa ni vyombo vya mawasiliano kama simu.

"Unapokilinda kifaa chako cha mawasiliano, tunasisitiza kuwa nywila yako (Password) ni siri yako wewe, si mke, mpendwa wako, mpenzi, mjomba, shangazi hapaswi kujua Nywila yako, kama mnapendana sana hapo nyumbani.

"Kama mna mapenzi ya dhati, mapenzi yasiyo tikisika, mapenzi imara, vyovyote utakavyo pamba hayo maneno Nywila haipaswi kushirikishwa mtu yeyote, nywila ni ya mmiliki wa kifaa cha mawasiliano, mtu yeyote hapaswi na halazimiki kujua nywila ya mtu mwingine, nwila yako ni usalama wako," amesema Robin Ulikaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live