Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mke amnunulia mdoli mumewe kumpunguza hamu ya mapenzi

Mdolii Mke amnunulia mdoli mumewe kumpunguza hamu ya mapenzi

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wanawake wengi wakiwa hawana mood ya kufanya mapenzi wanapata shida namna ya kuwaridhisha wanaume zao, lakini hii si kwa Charlotte Grey.

Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 23 amelazimika kununua mdoli wa mapenzi unaofanana nae ili uweze kumsaidia bwana’ake, Callum Black (28) katika mahusiano yao.

Hii ni kwa sababu jamaa huyo uwezo wake wa kufanya mapenzi ni mkubwa kuliko mpenzi wake na mwanamke hapendi sana mapenzi, hivyo kushindwa kuhimili mechi za kibabe toka kwa bwana'ke huyo.

Charlotte amesema awali hakuafiki suala la kuruhusu mtu mwingine mwingine aingie katika mahusiano yao ambayo wamedumu kwa miaka 15 sasa, sababu yeye angesikia wivu kama ilivyo kwa watu wengi.

Hivyo, ilibidi aongee na bwana'ke huyo wanunue mdoli anayefanana nae awe anamsaidia 'kazi' pale anapokuwa hajisikii wakati bwana'ke akitaka tendo la ndoa.

Charlotte ameongeza kwamba sababu ni mdoli wa plastiki hatosikia wivu tofauti ingekuwa ni mdada mwenzie kikwelikweli angejisikia wivu na kuleteana gubu.

Na ndio wakanunua mdoli mwezi June, mwaka huu kwa pesa ndefu na kuupa jina la Dee, wanauvalisha nguo za kuvutia, pia wanautoa out kwa gari na kwenda kutembea huku na huko ili usijihisi upweke au kutengwa ndani na nje ya nyumba.

Charlotte anadai tangu hapo anahisi mahusiano yao yapo salama na yamenogeshwa na doli hilo. Wawili hao wanaish London, nchini Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live