Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkasa wa kimapenzi wa Shakira na mtoto wa Rais

Shakira Mds Mkasa wa kimapenzi wa Shakira na mtoto wa Rais

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kabla ya Gerard Pique, Shakira alikuwa na mahusiano na Wakili kutoka Argentina, Antonio de la Rua tangu mwaka 2000 hadi Januari 2011 walipoachana rasmi.

Antonio de la Rua ni mtoto wa Rais wa zamani wa Argentina, Fernando de la Rua ambaye aliongoza nchi hiyo kutoka mwaka 1999 hadi 2001, na alikuwa mshauri wa Baba yake kipindi cha Urais. Mama yake anaitwa Ines Pertine.

Baada ya miaka 10 pamoja, Shakira na Antonio walitengana hapo Agosti 2010 katika kile walichoeleza ni uamuzi wa pande zote mbili lakini Antonio ataendelea kusimamia biashara na masilahi ya kazi za sanaa za Shakira kama ambavyo amekuwa akifanya.

Mwimbaji huyo wa Hips Don’t Lie, kupitia tovuti wake, Januari 10, 2011 alitangaza rasmi kuachana kwao na Antonio na kile walichokubaliana kwa pamoja.

“Tangu Agosti 2010 tumekubaliana kwa pamoja kuchukua muda kuwa mbali na mahusiano yetu ya kimapenzi, katika wakati wote tumeendelea kufanya kazi pamoja, tumebakia kuwa karibu na kuweka faragha masuala yote,”.

“Kwa pamoja tunakitazama kipindi hiki cha kutengana kama cha muda tu, na muda wa kila mmoja kukua huku tukiendelea kama washirika upande wa biashara,” alisomeka wakara huo wa Shakira.



Hata hivyo, Septemba 2012, Antonio alimshtaki Shakira kwa kudai fidia ya Dola100 milioni wastani wa Sh233.1 bilioni kwa kile alichodai alichangia sehemu kubwa ya mafaniko ya mwimbaji huyo. Lakini Agosti 2013 Mahakama ya Juu huko Los Angeles alitupilia mbali kesi hiyo.

Miongoni mwa dili ambazo Antonio alikuwa anadai kuzileta kwa Shakira ni ile na kampuni ya matamasha, Live Nation yenye thamani ya Dola300 milioni kwa kipindi cha miaka 10. Lakini kwa wakati wote Shakira alisema alifanya kazi na Antonio kama mshauri wake wa kibiashara na alilipwa kwa kazi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live