Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkapa awaliza Bongo Movie

Mkapa+pix Mkapa awaliza Bongo Movie

Sat, 25 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By CLEZENCIA TRYPHONEKUFUATIA kifo cha Rais Mstaafu wa Jamuhiri ya Muungano Tanzania, Benjamini Mkapa wasanii mbalimbali wakiwemo Bongo Movie ambao wameelezea hisia zao kwenye mitandao yao ya kijamii.

Hayati Mkapa amefariki usiku wa kuamkia leo Ijumaa katika akiwa anapatiwa matibabu hospitalini jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa wasanii waliotumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuandika maneno ya kuomboleza ni msanii wa vichekesho Lucas Mhavile 'Joti' aliyeandika hivi;

"Hakika Mwenyezi Mungu ndie mwenye kujua muda, siku, saa, Leo muda umefika kwake aliyekuwa Rais wetu wa awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa. RIP Mzee Wetu.MwenyeziMungu ametekeleza wajibu wake na wajibu huu lazima kila mwanadamu umkute ili neno lake Bwana litimie.

Joti ameongeza, "Nafasi pekee tuliyoibakiza hapa duniani ni Ibada tu, hakika hayo mengine ni mapito tu..Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi Amina,".

Naye Gabo Zigamba ameandika ''Busara za Taifa zimemfuata baba wa Taifa, nitakukumbuka daima, maneno yako mchakato, mkukuta, mkurabita, upembuzi yakinifu na utandawazi,''

Chanzo: mwanaspoti.co.tz