Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mkamata nyoka ang’atwa na nyoka na kufariki

Rubani Alazimika Kutua Baada Ya Kuona Nyoka Kwenye Kiti Chake Mkamata nyoka ang’atwa na nyoka na kufariki

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana mmoja nchini Uganda aliyejizoelea umaarufu mkubwa kutokana na shukhuli zake za ukamataji nyoka amefariki Dunia baada ya kung’atwa na nyoka wakati wa kazi zake.

Kwa mujibu wa Mkewe, Abdallah Kalule mwenye umri wa miaka 38, alimuona nyoka akiingia kwenye kichuguu kilichopo karibu na nyumbani kwake na kuamua kumfuata wakati wa harakati za kumkamata ndipo alipong’atwa na nyoka huyo kutoweka.

Mjomba wa marehemu ameongeza kuwa familia yao ina historia ya kukamata na kuwauza nyoka kwa kipindi kirefu ”Abdallah Kalule amekuwa akikamata nyoka kwa muda mrefu, baadhi yao ni wakubwa kuliko hata aliyemng’ata.

Hatuwezi kuendelea na biashara hatari kama hii ambayo inaweza kutufanya kupoteza maisha yetu,”

Marehemu, Abdallah Kalule hukamata nyoka hao na kuwauza kwa waganga wa jadi kwa kiasi cha tsh 93,466.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live