Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkali Wenu afunguka kuhusu kumtelekeza mama yake mzazi

Mkali Wenuuu Mkali Wenu afunguka kuhusu kumtelekeza mama yake mzazi

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji maarufu wa vichekesho na Bongo Fleva, Jackson Supakila Maarufu kama Mkali Wenu amefunguka kuhusu taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa amemtelekeza mama yake mzazi bila kumjali.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Mkali Wenu amekiri kuwa aliyehojiwa na vyombo vya habari na kusema hamjali kweli ni mama yake mzazi lakini kilichofanyika ni kuwa mama huyo alishawishiwa kuongea maneno hayo na hakujua madhara yake yatakuwa makubwa kiasi gani.

"Mama yangu alilazimishwa na kurubuniwa ili afanye ile interview… Hakuwa anajua kufanya vile kutaleta shida hata ndani ya familia. Wamekosea sana walioenda kumfanyia.

"Nililia sana nilipoona ile Interview, na hayo yote yamekuja mara baada ya Mimi kupewa gari. Wametumia mwanya huo kumjaza Mama uwongo, mimi ni masikini bado natafuta.

"Watu wengi wakiniona wanahisi Mimi ni tajiri sana, lakini ukweli ni kwamba sina pesa. Matatizo ya Mama yangu ni makubwa kuliko kipato changu.

"Wakati mwingine wabaya wanaotutengenezea visa na mikasa tunaishi nao ndani ya familia zetu ila mimi namuachia Mungu hayo yote,” alisema Mkaliwenu kupitia Wasafi FM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live