Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjukuu wa Bob Marley, Joseph Jo Mersa Marley afariki dunia

Aaaaaaa 1140x640.png Mjukuu wa Bob Marley, Joseph Jo Mersa Marley afariki dunia

Wed, 28 Dec 2022 Chanzo: dar24

Kwa mujibu wa TMZ ambao ni miongoni mwa vyombo vya kwanza kutoa taarifa ya kifo hicho, Joseph, maarufu Jo Mersa, alifariki Jumanne Desemba 27, 2022 kutokana na matatizo yanayohusiana na pumu, ingawa maelezo ya kina kuhusu kifo chake bado hayajawekwa wazi.

Joseph, ambaye ni mtoto Stephen Marley, muda mchache uliopita alijiunga na chuo cha Miami Dade na kusoma uhandisi wa sauti (audio engineering) baada ya kukaa miaka yake kadhaa huko Jamaika.

Mwaka 2014 aliachia Ep yake iliyoitwa “Comfortable”, ambayo ilikuwa na nyimbo kama vile “Rock and Swing” na “Bogus.” Pia alitoa wimbo uliovuma sana, “Burn It Down,” mwaka wa 2016 na mwaka jana alifanikiwa kualiachia Ep yake ya 2, “Eternal,”.

Joseph amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 31 tu.

Chanzo: dar24