Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjomba: Serikali iunge mkono muziki wa asili

48cc8c7b0787697bc25b5a1bafc391a6 Mjomba: Serikali iunge mkono muziki wa asili

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa kughani mashairi nchini, Mrisho Mpoto 'Mjomba' ameiomba serikali kuwaunga mkono wanamuziki wanaoimba muziki wenye asili ya utamaduni wa Kitanzania.

Mpoto alitoa kauli hiyo, Dar es Salaam juzi baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi alipozungumza na wasanii wa muziki.

Alisema kuna changamoto ya soko kwa wasanii wanaofanya muziki wenye mahadhi ys nyumbani mashabiki hawazipendi kwa sababu wanapenda nyimbo zenye maadili ambayo siyo ya kitanzania.

"Muziki wa kukopi una mashibiki wengi lakini hazina asili ya maadili ya kitanzania, kwa sababu wanaofanya muziki wa kitanzania hawaungwi mkono mwisho wa siku tunaacha utamaduni wetu," alisema.

Mpoto alisema hata vikundi vya ngoma za asili ambavyo ni muhimu watu wanaacha kucheza kutokana na kwamba hawaungwi mkono kabisa.

"Vikundi vya ngoma ni muhimu kwenye shughuli za kiserikali hususani wanapokuja wageni wa kitaifa, badala ya kuwakusanya watu na kucheza hatuwezi kupata asili inayokubalika lakini kuna haja kwa serikali kutenga bajeti kwa ajili ya vikundi vya ngoma na kuviwezesha kiuchumi," alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz