Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjadala kifo cha Mohbad wafungwa rasmi

Polisi Hawajapata Ripoti Kifo Cha Mohbad Mohbad.

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusubiri majibu ya vipimo ya mwili wa mwanamuziki kutoka Nigeria Mohbad kwa miezi nane sasa, Daktari Bingwa wa Uchunguzi wa Kisayansi na Patholojia kutoka Hospitali ya Taaluma ya Chuo Kikuu cha Jimbo la Lagos (LASUTH), Prof. Shokunle Shoyemi ameeleza kuwa chanzo cha kifo cha msanii huyo hakiwezi kutambulika.

Kwa mujibu wa tovuti ya Hammer times na vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeeleza kuwa Prof. Shokunle Shoyemi alitoa maelezo hayo siku ya jana Jumatano Mei 15 mbele ya Mahakama kwa kuweka wazi kuwa sababu ya kifo cha Mohbad hakikuweza kufahamika kutokana na mwili huo kufanyiwa uchunguzi ukiwa umeharibika.

Prof. Osiyemi alimweleza Hakimu Adedayo Shotobi, kuwa chanzo cha kifo hakikuweza kufahamika kutokana na kuchukua takribani siku 21 kabla ya uchunguzi wa maiti kufanyika kwa muda huo mwili ulikuwa tayari umeshaharibika.

Shokunle pia alimuelezea hakimu kuhusiana na msanii kutokwa na damu baada ya kifo chake ambapo alidai kuwa madai hayo yalikuwa ni ya uongo.

Mwanamuziki huyo alifariki Septemba 12, 2023 na kuzikwa siku iliyofuata, kifo cha msanii huyo kilizua utata na kusababisha Serikali katika Jimbo la Lagos kufanya uchunguzi huku mwili wake ukifukuliwa kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi huo ambao ulianza Oktoba 13 mwaka jana, katika Mahakama ya Mwanzo ya Ikorodu.

Hata hivyo, kesi hiyo iliahirishwa kwa siku ya jana mpaka Juni 11 mwaka huu, huku uchunguzi ukiendelea kufanyika. Kupitia kesi hiyo watu mbalimbali walikamatwa ambao walikuwa wakihusishwa na kesi hiyo mmojawapo akiwa ni bosi wake wa zamani Naira Marley, Sam Larry, na rafiki yake wa karibu Primeboy, lakini watu hao walifanikiwa kutoka kwa dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live