Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjadala gari la Diamond na ukweli kuhusu magari ya bei mbaya

Diamondpicccc Data Mjadala gari la Diamond na ukweli kuhusu magari ya bei mbaya

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Achana na ule mjadala ulioshika kasi katika mitandao ya kijamii kuhusu gari aina ya Cadillac Escalade Sky Captain alilonunua msanii wa Tanzania, Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz.

Wapo wanaosema gari la msanii huyo si jipya na wengine wakidai ni jipya huku bei halisi ya gari hilo ikiibua mjadala miongoni mwa watu wanaomfuatilia.

Wakati bei ya Cadillac Escalade Sky Captain ikiwa kati ya Sh800 milioni hadi Sh1.1 bilioni, ukweli ni kwamba gari ya gharama zaidi duniani ni Ferari ambayo inatengenezwa nchini Italia.

Ferari

Gari hilo lilivumbuliwa na Enzo Ferrari mwaka 1939 kama magari ya mashindano. Kwa gharama ya sasa, gari hilo aina ya Ferrari 250 GTO linauzwa dola 70,000,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh162.5 bilioni.

Gari linalofuata kwa kuuzwa bei kubwa ni Bugatti La Voiture Noire ambalo bei yake ni dola 18,700,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh43.4 bilioni.

Miongoni mwa wanaomiliki gari hilo ni pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo.

Pagani Zonda HP Barchetta

Linalofuatia ni Pagani Zonda HP Barchetta linalouzwa dola  17,600,000 za Marekani sawa na Sh40.7bilioni. Gari hilo lililotengenezwa kwa ajili ya mbio za magari lilianza kutengenezwa tangu mwaka 1991 nchini Italia.

Namba nne inashikiliwa na Bugatti Centodieci linalouzwa dola 9,000,000 sawa na Sh20.8 bilioni. Gari hilo lililobuniwa na Achim Anscheidt na linatengenezwa nchini Ufaransa katika mji wa Molsheim.

Bugatti Centodieci

Gari namba tano kwa kuuzwa bei mbaya ni Bugatti Divo ambalo ni dola  6,000,000 za Marekani sawa na Sh13.9 bilioni likifuatiwa na Bugatti Chiron Super Sport linalouzwa Dola 5,740,000 za Marekani sawa na Sh13.3 bilioni.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz