Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miwani zenye saini ya Diddy zasitishwa kuuzwa

Diddy Akabiliwa Na Msala Mwingine P.Diddy

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya America's Best Contacts & Eyeglasses imeripotiwa kusitisha kuuza fremu za miwani zenye saini ya Diddy kutokana na kuhusishwa kwenye kesi kadhaa za unyanyasaji wa ngono.

Kwa mujibu wa Tmz taarifa hiyo imethibitishwa na mwakilishi wa kampuni hiyo kwamba maduka hayo yalianza kuacha kuuza fremu zenye saini ya Diddy Jumanne iliyopita huku zikiuzwa za kawaida ambapo mpaka sasa haijawekwa wazi kuwa fremu hiza za Combs zitapelekwa wapi.

Ingawa kampuni hiyo haikufichua sababu kamili ya hatua hiyo, lakini kilingana na wadau mbalimbali wamedai kuwa uamuzi huo unahusishwa wazi na hisia za umma kufuatia na video iliyosambazwa wiki iliyopita ikimuonesha Diddy akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie.

Mpaka kufiki sasa Diddy amehusishwa kwenye kesi saba za unyanyasaji wa kingono huku ya mwisho ikifunguliwa siku tatu zilizopita na aliyekuwa mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Mitindo aitwaye Lampos.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live