Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitandao inaendesha ndoa za mastaa au ndoa zinaendesha mitandao?

46995 Pic+ndoa

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zamani zilikuwapo hadithi kuwa watu maarufu majuu walikuwa na ndoa za mkataba. Mfano ni ndoa ya waigizaji Willy Smith na mkewe Jada Pinkett au Michael Jackson na Debbie Row.

Jay Z na Beyonce nao wamekuwa gumzo kuhusu ndoa yao ingawa wao wamekuwa wasiri sana. Watumiaji wa mitandao wmejaribu kupenya ndani ya ndoa hiyo lakini imetoka kapa.

Ingawa wanamuziki hao matajiri wamewahi kupitia katika kipindi kigumu cha ndoa yao, hajawahi kusema nini kiliwagonganisha, tofauti na Rapa Cardi B ambaye akichefuliwa na mpenzi wake Off Set, kitu cha kwanza anachofanya ni kujirekodi na kuweka katika mtandao wa Instagram.

Wapo wasanii nchini wanafahamika kuwa ndani ya ndoa, lakini kinachoendelea katika maisha yao havipo kwenye mtandao. Inspector Haroun, Joti, Mwana FA, AY na Mheshimiwa Temba ni baadhi walioweka maisha yao ya ndoa nje ya mtandao.

Nani hafahamu kuhusu ndoa za Nuh Mziwanda na Nawal, Irene Uwoya na Dogo Janja, Shilole na Uchebe, Shamsa Ford na Chid Mapenzi au Wastara na ndoa zake? Kila anayefuatilia masuala ya mtandao huenda anafahamu jambo moja au mawili kuwahusu.

Hivi karibuni limezuka jipya la ndoa ya mwanamuziki H Baba na mkewe Florah Mvungi na katika hali ya kustaajabisha mume anasema madai ya mkewe yanalenga kufurahisha wanazengo mtandaoni.

Florah anasema ndoa yake imevunjika miaka mitatu iliyopita kwa mara ya kwanza wiki hii baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu kwamba wawili hao wameachana.

Katika mahojiano yake na Mwananchi, Flora alisema amechoka kuulizwa maswali hayo mara kwa mara na sasa ameamua kuweka wazi kuwa ni kweli wameachana. Mwigizaji huyo ambaye alipata umaarufu kupitia kipindi cha TV cha ‘Bongo Dar es Salaam’, anasema aliachana na mumewe huo miaka mitatu iliyopita, lakini aliamua kukaa kimya kutokana na sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.

Alipoulizwa chanzo cha ugomvi wao hasa ni nini hadi kufikia hatua ya kutengana huku wakiwa tayari na watoto wawili, Flora anasema hawezi kusema H Baba ndiye mwenye makosa au yeye ila watu wajue tu wameachana na yeye siyo wa kwanza wala wa mwisho ndoa kuvunjika.

Kwa upande wake H Baba ambaye aliwahi kutingisha na wimbo wa ‘Mpenzi Bubu’ alipotafutwa ili kujua ukweli wa jambo hilo, anasema asingependa kuzungumzia habari za ndoa kwani mkewe hakumuolea kwa waandishi wa habari wala kwenye Instagram.

“Siwezi kuachana na mke wangu kwa Instagram, kama nilivyofuata taratibu wakati namuoa ndivyo nitakavyofanya wakati ikifika wa kuachana naye lakini mtambue kwamba Flora bado ni mke wangu na ninampenda sana hicho anachokiongea huwezi kujua labda ni hizo promo za Bongo movie zao,” anasema H Baba ambaye asili yake ni mzaliwa wa Mkoani Mwanza. “Binafsi sipendi kuzungumzia masuala ya familia kwenye mitandao huwa siyapendelei na sijalelewa hivyo muulizeni vizuri awaonyeshe talaka ya kuachwa.”

Pia, wakati anasema wameachana miaka mitatu iliyopita ukweli ni kwamba mtoto wao mdogo ana miaka mitatu, na kuhoji walimpataje kama walikuwa wameachana.

Kuhusu watoto anasema yupo nao na shule wanasoma Dar es Salaam, ila yupo Mwanza kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa nyumba yao na kueleza mikakati ilikuwa ni Flora kumfuata baada ya kumaliza chuo.



Chanzo: mwananchi.co.tz