Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miss awachanganya Diamond na Ben Pol

Ben Pol Diamond Ben Pol na Diamond

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alianza kuimba tangu akiwa shule wakati anasoma ekondani ndipo akajiunga na Tanzania House of Talents (THT) ila alitoka kimuziki chini ya M Lab (Music Laboratory) na sasa ni miongoni mwa waimbaji wakali wa RnB Bongo.

Ben Pol ametoa albamu mbili, EP moja, ameshinda Tuzo za Muziki Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo, amefanya kolabo na wasanii wa kimataifa na ameshiriki miradi mikubwa katika muziki kama Coke Studio Africa. Mfahamu zaidi:

1. Alipozaliwa alipewa jina la ‘Majuto’ kutokana na kuzaliwa wakati baba yake akiwa amefungwa jela miaka miwili, na jina hilo lilikuja alipoenda kumtembelea baba yake gerezani Keko akiwa na siku 40 tu tangu kuzaliwa, ila alipobatizwa ndipo akaitwa Bernad.

2. Rapa Stereo ni miongoni mwa watu wa mwanzo kumwambia Ben Pol kuwa ana uwezo mkubwa kimuziki wakati wanasoma Dar es Salaam Secondary School na akamshauri kwenda THT.

Na baadaye wakaja kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya M Lab. Wimbo wa kwanza kuachia pamoja unaitwa ‘Pata Raha’ ambao Nikki Mbishi na One The Incredible walishirikishwa pia.

3. Prodyuza Duke Tachez alimwambia Ben Pol anampa ofa ya kurekodi wimbo mmoja aliporekodi ‘Pata Raha’ vizuri akampa ofa ya kurekodi ngoma 10 na ndipo Ben Pol akatoa ngoma kama Nikikupa, Maumivu, Number One Fan, Samboira na nyinginezo ambazo zilimtoa kimuziki.

4. Mtu wa kwanza maarufu Bongo Ben Bol kufurahia baada ya kumfuata (follow) yeye Instagram ni mtangazaji Salama Jabir ambaye alimuimba kwenye wimbo wake, Jikubali.

5. Chini ya THT, Ben Pol na Zamaradi Mketema ni maproduza wa filamu Wrong Number waliocheza kina Monalisa, Hemedy PHD na Garner G Habash na huu ulikuwa mradi wa Ruge Mutahaba.

Hata hivyo, akiwa shule ya msingi Ben Pol alicheza filamu yake ya kwanza na kina Bi. Shanga na ilishutiwa Pugu.

6. Ben Pol alienda kuomba nafasi ya kusaini lebo studio kwa Man Water lakini akakosa nafasi, ila aliposhinda shindano la kuimba redioni la ‘Nyuki DJ’ akapewa nafasi ya kurekodi kwa Man Water na waandaaji wa shindano hilo.

7. Ben Pol amefanya video na wanawake wawili ambao amewahi kuwa nao katika mahusiano. Kuna Ebitoke aliyetokea kwenye video ya wimbo Natuliza Boli, huku Anerlisa kutokea nchini Kenya akitokea kwenye video ya wimbo ‘Kidani’.

8. Filamu zenye matumizi ya bunduki na mabomu kwa sana Ben Pol huwa hapendi kuzitazama na vyakula vyenye pilipili kwa wingi havipendi kabisa!

9. Mrembo anayeonekana kwenye video ya wimbo wa Ben Pol wa Phone anaitwa Lucy Charles ambaye ni Miss Mwanza mwaka 2013. Pia mrembo huyo ndiye ametokea kwenye video ya wimbo wa Diamond Platnumz wa Sikomi.

Utakumbuka mwaka 2013 taji la Miss Tanzania lilienda kwa Happiness Watimanywa, binti wa miaka 19 wakati huo ambaye pia alitwaa taji la mrembo mwenye mvuto kwenye picha (miss photogenic).

10. Ben Pol ndiye msanii pekee Bongo mwenye historia kubwa kwenye muziki wa Darassa, mosi; wimbo wa kwanza kumtoa Darassa kimuziki ‘Sikati Tamaa’ Ben Pol ndiye aliyeimba kiitikio chake.

Pili; wimbo wa Darassa wenye mafanikio makubwa zaidi ‘Muziki’ Ben Pol ndiye alihusika kwenye kiitikio na ni wimbo wa rapa huyo ambao video yake inaongoza kwa kutazamwa zaidi YouTube ukiwa na views zaidi ya milioni 21 tangu kuachiwa miaka minne iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live