Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miss Utalii yarejea, waandaaji lazima kuwa na ‘degree’

65318 Pic+utalii

Wed, 3 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shindano la Miss Utalii nchini Tanzania  limerejea ikiwa imepita miaka sita tangu lilipozuiwa kufanyika.

Hivi sasa waratibu wa ngazi ya kanda wa shindano hilo wanatakiwa kuwa na elimu kuanzia shahada ili kupatiwa kibali cha uandaaji.

Hayo yameelezwa jana Jumanne Julai 2, 2019 na mwenyekiti mtendaji wa bodi ya mashindano hayo, Gidion Chipungahelo maarufu  'Chips' alipotembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communication’s Ltd (MCL) zilizopo Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya Chipungahelo imethibitishwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kupitia msemaji wake,  Agnes Kimwaga.

Mashindano hayo yalifungiwa mwaka 2013 na Basata kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutakiwa kuendeshwa kama taasisi na si mtu mmoja kama alivyokuwa ikifanyika.

Huku akieleza jinsi shindano hilo lilivyoboreshwa, Chips amesema sasa litaendeshwa na wasomi ili kuleta tija zaidi.

Pia Soma

“Nashukuru Basata kutufungulia kwa wakati muafaka. Katika kuliboresha zaidi shindano hili litafanyika kitaifa mwezi Desemba badala ya Novemba. Itakuwa siku ya mkesha kuamkia sherehe za Uhuru, Desemba 8,2019” amesema Chips.

Chanzo: mwananchi.co.tz