Idara ya Uhamiaji nchini Afrika ya Kusini imeamua kumnyang’anya utambulisho wa uraia Mrembo wa Afrika ya Kusini, Chidimma Adetshina baada ya kugundua amefanya udanganyifu wa uraia wake.
Agosti mwaka huu, Chidimma Adetshina alishinda taji la urembo la “Miss Universe South Africa” ambapo ushindi wake ulizua mjadala kuhusiana na uraia wa wazazi wake ambapo mama ni raia wa Msumbiji na Baba mzazi Mnigeria.
Idara ya Uhamiaji nchini humo ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa mrembo huyo hana uraia wa Afrika ya Kusini.
Chidimma Adetshina alikuwa ni mwanasheria ambaye alishinda taji la Miss Universe Nigeria baada ya kushiriki shindano la Miss South Africa.