Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miss Tanzania awanogea WCB

Miss Tz Pic Data Miss Tanzania awanogea WCB

Sat, 27 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MISS Tanzania namba mbili 2018, Nelly Kazikazi ameonekana kuwanogea wasanii wa lebo ya WCB, baada ya kumtumia mara ya tatu katika video zao.

Nelly aliyewahi kuwa video vixen kwenye wimbo wa Nisamehe wa Zuchu kwa mara ingine ameonekana kwenye video ya Yalah ya msanii Mbosso kutoka lebo hiyo.

Yalah ni moja ya wimbo uliopo katika albamu ya msanii huyo ya ‘Definition of Love’, video hiyo iliachiwa wiki hii na tayari imetazamwa zaidi ya mara milioni moja hadi sasa.

Ukiachilia wimbo wa Nisamehe na Yalah, kwa mara ya kwanza alionekanna kwenye wimbo wa Kilio wa Lavalava ulitoka miaka mitatu iliyopita.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nelly alisema mchongo wa kuwa karibu na wasanii wa lebo hiyo ulitokana na Lavalava aliyemtafuta kufanya naye kazi.

“Mpaka leo najikuta ni kama mmoja wa familia ya WCB, imetokana na kuunganishwa na msanii Lavalava ambaye niliwahi kufanya naye kazi kama hiyo ya video vixen kwenye wimbo wake wa Kilio, hii ni baada ya kutumwa na muongozaji wa video, Kenny anitafute,” alisema Nelly ambaye pia ni balozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz