Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miss Tanzania asepa Miss World

Miss Tzz(1) Miss Tanzania asepa Miss World

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Halima Kopwe Hatimaye jana ameondoka rasmi Tanzania kuelekea nchini India kwa ajili ya mashindano ya Miss World yanayotarajia kufanyika kuanzia Februari 18 mpaka Machi 9,2024.

Halima amesema hayo wakati akiagwa kwenda kuiwakilisha Nchi katika mashindano hayo makubwa huku akisema “Miss Tanzania imenisaidia sana mambo mengi, na ahaidi nitafanya kila lililopo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha narudisha heshima ya Miss Tanzania Kwenye jukwaa la Miss World”.

Itakumbukwa Halima alitakiwa kwenda Miss World mwezi May mwaka 2023 ambapo ilitakiwa kufanyika Falme za kiarabu na kuahirishwa kupelekea India ambapo ilitakiwa kufanyika Desemba 12, 2023 lakini kutokana na sababu za kiafya wakasogeza mbele mpaka mwezi huu Februari hukohuko India na fainali zikitarajiwa kufanyika Machi 09, 2024.

Chanzo: Mwanaspoti