Mrembo aliyeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss World, Elizabeth Makune amezitaja sababu za kushindwa kutwaa taji hilo kuwa ni wananchi na kamati ya shindano hilo.
Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalumu kwa mara ya kwanza tangu arudi kwenye shindano hilo nchini China, Elizabeth amesema si nchi wala kamati ya mashindano hayo waliokuwa wamejipanga kuhakikisha anarudi na ushindi.
Mkurugenzi wa Kampuni inayoanHata hivyo daa shindano la Miss Tanzania ‘The Look’ Basila Mwanukuzi alisema wao wamefanya kazi yao kama watayarishaji.
“Sisi hatuna chombo cha kutangaza kuwaambia wananchi wampigie kura, kila Mtanzania alitakiwa aguswe popote pale alipo halikupaswa kuachiwa Basila peke yake, kamati au mshiriki , ”alisema Mwanukuzi.
Elizabeth alitoa mfano kwenye upigaji wa kura kamati ilikuwa haina utaratibu wa kuhakikisha inawafahamisha wananchi nini cha kufanya hadi walipoona kwenye mitandao.
“Zile nguvu zilizotumika kupiga kura dakika za lala salama zingetumika wakati wa shindano sasa hivi tungekuwa tunazungumzia ushindi.”