Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miss Tanzania alamba shavu Bodi ya Utalii

49527 Pic+miss

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tanzania, Queen Elizabeth Makune amelamba dili la kuwa balozi wa Bodi ya Utalii nchini ikiwa harakati za kumtafuta mrithi wake zimeanza kushika hatamu nchini.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini, Devota Mdachi amesema lengo la mkataba huo ni kumwezesha kutangaza vivutio vya utalii nchini.

“Kama mnavyofahamu Bodi ya Utalii imekuwa ikidhamini Miss Tanzania na kuandaa ziara mbalimbali za kuwatembeza warembo na kuwaonyesha utajiri wetu wa maliasili, tuliwatembeza pori la akiba la Selous na msitu wa asili wa amani,” amesema.

Amesema anaamini i atasimama kuwaeleza Watanzania umuhimu wa kuwa watalii ndani ya nchi na pia kuwaeleza wageni utofauti wetu na wengine duniani.

Mdachi amesema mkataba huo ni wa mwaka mmoja na litakwenda kwa mrembo atakayeibuka mshindi wa Miss Tanzania kwa mwaka huu.

Naye Elizabeth ambaye ni Miss Kinondoni pia, amesema ataitumia nafasi na umaarufu wake katika jamii kuinadi nchi ndani na nje ya nchi.

“Ninataka kuwa mfano kwa sababu nimepewa kazi ambayo ni muhimu kwa Taifa. Ninatumia kila dakika yangu vizuri kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz