Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miss Kanda ya Mashariki kulamba shilingi milioni mbili

16406 Miss+Tanzania+pic Miss Kanda ya Mashariki kulamba shilingi milioni mbili

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Mshindi wa mashindano ya Miss Kanda ya Mashariki kuondoka na kitita cha Sh2 milioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Septemba 15, 2021 na mratibu wa mashindano hayo, Nancy Matta, kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo,yatakayofanyika Septemba 24.

Nancy amesema mashindabo hayo yanayotarajiwa kufanyika mkoani Morogoro, yatashirikisha warembo 16 na atakayeibuka mshindi atalamba kiasi hicho cha Sh2 milioni na kuvalishwa taji lenye thamani ya Sh3 milioni.

"Ukiachilia mbali mshindi kupata zawadi hiyo,pia mshindi wa pili atapata Sh1.5 milioni huku mshindi wa tatu ataondoka na sh1 milioni na washiriki wengine kujipatia kifuta jasho cha Sh100,000 kila mmoja," amesema  Nancy.

Kwa upande wao Bodi ya Utalii (TTB), ambao ni moja ya wadhamini wa mashindano hilo,amesema kipindi cha kuwa kambini washiriki hao watakwenda kutembelea vituo mbalimbali vya utalii.

Maria Mafie ambaye ni Ofisa Utalii wa TTB, amesema anaamini kwa kufanya hivyo washiriki watajifunza na kwenda kuutangaza utalii nje ya nchi mmojawapo atakapobahatika kuwakilisha nchi katika mashindano ya dunia.

Mashindano Kanda ya Mashariki yanahusisha warembo kutoka mikoa ya Lindi, Pwani, Mtwara na Morogoro na yatafanyika hoteli ya Morena mkoani Morogoro.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz