Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Miss Ivory Coast: Adingra anapaswa kuzawadiwa kitu

Simond Adingra Kouassi Miss Ivory Coast: Adingra anapaswa kuzawadiwa kitu

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi wa Taji la Miss Ivory Coast mwaka 2022, mrembo Marlène Kouassi Kany (25) amesema kwa sasa anatamani kukutana na mshambuliaji wa Kimataifa wa nchi hiyo, Simon Adingra (22), baada ya kuvutiwa na Kiwango bora alichokionesha katika michuano ya AFCON 2023 na kilichosaidia Taifa lake kuibuka na ubingwa.

Mrembo huyo ameongezea kwa kusema nyota huyo anahitaji pongezi kubwa kutokana na juhudi zake uwanjani hivyo hawezi kumuacha hivi hivi.

Tangu kutamaika kwa michuano hiyo, Simon Adingra amekuwa hakauki kwenye midomo ya Waivory Coast na kumezewa mate na warembo, hata kuonekana kana kwamba yeye ndiye kipenzi kipya cha wanawake nchini humo.

Simon Adingra alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi ya fainali ya dhidi ya Nigeria, amemaliza michuano hiyo akifunga bao moja na kutoa Assist mbili kwenye mchezo wa fainali.

Adingra ambaye anakipiga katika Klabu ya Brighton & Hove Albion F.C ya nchini Uingereza, ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa michuano ya AFCON iliyokuwa ikitimua vumbi nchini kwao Ivory Coast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live