Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miss Bantu: Nataka mwanaume wa miaka 50-60

Miss Bantu Miss Bantu: Nataka mwanaume wa miaka 50-60

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo maarufu Bongo, Miss Bantu ameswema kuwa kwa sasa anatafuta mwanaume wa kumuoa mabye ni mtu mzima kwani vijana wengi wamekuwa wasubufu kwenye mahusano ya kimapenzi.

Miss Bantu amesema kuwa anataka mzee mwenye umri mkubwa kwani ameshapitia mengi na kujifunza hivyo itakuwa vizuri kuendana naye na kuishi pamoja kwa upendo na amani kulivyo kijana mwenye umri mdogo.

"Mimi nataka mwanaume mwenye umri kuanzia miaka 50 mpaka 60 na kuendelea kwa sababu watu wa aina hiyo tayari wameshapitia vitu vingi wameamua kutulia, wanajua kujali, kuhonga ndio usiseme, siwezi kudeti na vijana majibaba wananitosha, masiposa ndiyo habari ya mjini.

"Wazee hawana stress ila hawa vijana wadogowadogo unaweza ukafa na presha bora upate kibaba chako cha miaka 60, kwanza saa mbili amelala anakupigia simu saa ngapi!. Vijana wengi wanajisifia kufanya mapenzi lakini hawana pesa.

"Sasa tutakula nyasi au! bora nibaki na mzee pesa ina nguvu sana, nikiwahi kuhongwa milioni 20 na mzee ambaye ni mzazi mwenzangu , ningekuwa na kijana asingenipa hiyo pesa," amesema Miss Bantu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live