Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misosi awaumbua wasanii walozi

78f4a66f33d1d98b2845f5121aebe0a6 Misosi awaumbua wasanii walozi

Mon, 31 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ amefunguka baadhi ya wasanii wanautamaduni wa kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata mafanikio katika muziki.

Bwana Misosi aliyewahi kutamba na kibao cha ‘Mabinti wa Kitanga’ alisema ushindani unaoendelea kukua kila kukicha kwenye tasnia hiyo kwa sasa ni miongoni mwasababu zinazowafanya wasanii wengi wakiwemo hata wale wanaochipukia kwenda sehemu hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi Bwana Misosi alisema kila msanii anahitaji kila kibao anachoachia kipate mwitikio mkubwa sokoni, hivyo hawaamini ubora wa kazi zao na badala ya kumtegemea Mungu, wenyewe wanaamini kwa waganga ili kuongeza kazi zao.

“Sio jambo la kushangaza tasnia imekuwa ngumu kutokana na kila shabiki anapenda kusikiliza kazi nzuri na kutokana na ugumu huo kuna baadhi ya wasanii wanaenda kwa waganga kutafuta nyota,” alisema Bwana Misosi

Bwana Misosi amewaomba kufanya kazi zenye ubora unaozingatia weledi wa maudhuni ni kipimo tosha kinachoweza kumbeba katika kazi zake kupendwa, lakini kama wasanii wataendelea kuamini kwenda kwa waganga kunaweza kuwatoa, basi sanaa itaendelea kubaki historia kuelekea kwenye mafanikio.

Chanzo: habarileo.co.tz