Mtangazaji mkongwe Miriam Migomba, atangaza kuondoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuhudumu kwa muda mrefu wa miaka 20 toka 2004 hadi mwaka huu 2024.
Migomba anakuwa ni mtangazaji wa pili ndani ya wiki moja kuacha kazi baada ya Djaro Arungu kufanya hivyo wiki iliyopita.
"Naitwa Mariam wa Migomba ‘mammy Orijinali’ wengi wamezoea kuniita namna hiyo. Kwa masikitiko makubwa sana, sina namna, inabidi niweke wazi ili mashabiki zangu waliokuwa wakinisikiliza kwenye Sasambu wajue.
"Utangazaji wangu nilianza mwaka 2004 mpaka 2024, sina namna, sina budi, lazima hiki kitu nikiongee na nikieleze. Kuanzia leo, mimi sio tena mwanafamilia wa TBC FM," amesema Miriam.