Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miracle Baby: Mtu asiniulize kuhusu baba'ngu, sikujizaa

Miracle Baby Miracle Baby

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi karibuni mitandao ya kijamii nchini Kenya ilisambazwa na video ya mzee mmoja aliyejitokeza akidai kwamba ni babake msanii wa Mugithi Peter Miracle Baby.

Mzee huyo alisema kwamba kijana huyo aliyeuwa kiongozi wa kundi la Gengetone Sailors Gang ni mtoto wake na kwa jina kamili anaitwa Willy Mpole.

Mzee alizidi kuelezea kwamba alimzaa katika maeneo ya Mathare sehemu inaitwa Mlango Kubwa. “Mimi ndio babake Miracle Baby anaitwa Willy Mpole nilimzalia hapa Mlango Kubwa,” mzee huyo alisema.

Alimtaka msanii huyo kumkwamua kutoka kwa lindi la umaskini wa mtaa wa mabanda wa Mathare na kumweka katika maisha angalau yenye tija.

Baada ya video hiyo kusambazwa mitandaoni, msanii Miracle Baby hatimaye amefunguka kuhusu ishu nzima na ameonekana kuchukua mkondo wa Ommy Dimpozw a kukana kabisa kwamab hamjui huyo mzee.

Miracle Baby kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema kwamba yeye hana uwezo wa kumtambua kama babake kwani ukweli ni kwamba anayejua baba ni mama pekee.

“Niseme Nini mimi Willy Mpole na msee mwingine asiniulize kuhusu babangu tena kwani coz sikujizaa mimi na amjuae baba ya mtoto ni mama so io swali si yangu kujibu,” Miracle Baby alisema.

Watu wengi walionekana kumuunga mkono msanii huyo katika suala hilo kwa kusema kwamba kumekuwa na mripuko wa kina baba wanaowatelekeza watoto wao kisha baadae nyota zao ziking’aa baba hawa wanajitokeza wakitaka kuteleza kwa ganda la ndizi la watoto hao.

Sakata hili linajiri huku nchini Tanzania msanii Ommy Dimpoz akiwa katika mzozo mkali mitandaoni baada ya klipu kuibuka kwamba yeye na babake hawala kutoka sahani moja na mzee wake sasa anataka kutambulika kama babake licha ya kumtelekeza awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live