Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Mimi ni mbahili, situmi na yakutolea"-Msami Baby

MSAMI.png "Mimi ni mbahili, situmi na yakutolea"-Msami Baby

Tue, 12 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na mkali wa kucheza hapa nchini Msami Baby, amefunguka kusema yeye ni mbahili sana kwenye matumizi ya pesa, pia huwa hatumi ya kutolea pale mtu anapomuomba msaada wa kumtumia pesa.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Msami Baby amesema hana matumizi makubwa na hatembeagi na pesa mfukoni mara nyingi huwa anatumia kadi au kufanya miamala kutumia njia ya simu.

"Mimi sio mtu wa kutembea na Cash napenda kutumia kadi na miamala mingine kwenye simu, kwa hiyo kilichokuwepo kwenye akaunti yangu ndicho naweza kufanya matumizi au ku-deal nacho, na kwenye matumizi inategemea naenda wapi, kwa tukio gani au mazingira ambayo nipo" amesema Msami Baby.

"Napenda kuishi kwa bajeti halafu mimi ni mbahili sana, pesa yangu haitumiki hovyo situmi na yakutolea, ukiniambia nitume kiasi nitatuma hichohicho ambacho tumekubaliana kama utataka ya kutolea itabidi uweke kwenye maongezi yetu kabla, ila mambo ya kujiongeza na kutolea huwa sina". ameongeza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live