Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Mimi ndiyo rapa ninayeingiza pesa nyingi" - Wizzy

Wizzy Webs "Mimi ndiyo rapa ninayeingiza pesa nyingi" - Wizzy

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Rapa Country Wizzy amesema ametimiza miaka 10 kwenye mziki na moja ya kitu alichojifunza ni kuchukua elimu ya biashara ya mziki ambapo amekua ni mmoja wa wasanii wanaongiza pesa nyingi kupitia Digital Platform. 

"Nimekaa zaidi ya miaka 10 kwenye mziki, nimejifunza vitu vingi sana hasa kibiashara. Nimesomea miaka mitatu biashara ya mziki namna ya kuingiza pesa kwa kutumia Digital Platform."

"Nimebahatika kuwa rapa ninayeingiza pesa nyingi kila mwisho wa mwezi, ni pesa ambayo pengine wasanii wengine hawaingizi, najiona mkubwa kuuza kazi zangu na kuniingiza kipato kikubwa," ameongeza Country Wizzy   

Chanzo: Eatv