Usiku wa kuamkia jana Mwigizaji Staa wa Bongo Movie nchini, Irene Uwoya amezindua filamu yake mpya inayoitwa OLEMA, filamu hiyo imezinduliwa jijini Arusha katika ukumbi wa Regalz Cinema.
Akiidadavua filamu hiyo, Uwoya amesema kwanza ameishuti kwa muda wa miaka miwili na imetumia zaidi ya milioni 180 za Kitanzania.
Amesema mazingira ya kutengeneza filamu hiyo yalikuwa magumu kutokana wa wahusika wengi hasa wamasai walikuwa hawajawahi kuigiza na hiyo ndiyo ilikuwa mara yao ya kwanza.
Lakini pia baadhi ya wahusika walikuwa hawajui kuongea Lugha ya kiswahili hivyo ilimpa ugumu sana. Irene Uwoya pia amekiri kwamba yeye ni Mmasai kabisa damudamu kwasababu baba yake alikuwa Mmasai.
Na Kuhusu mahali itakapoonyeshwa filamu hiyo, Uwoya amesema kuhusu hilo watu wasubiri kidogo mpaka hapo atakapowatangazia, lakini jicho lake hasa linaangazia kuipeleka filamu hiyo Netflix na anaamini milioni 180 alizotumia kushutia Filamu hiyo zitarudi mara dufu.