Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mimi Mars: Hakuna kitu kibaya kama upweke, natamani mpenzi

Mimimmarsz Mimi Mars: Hakuna kitu kibaya kama upweke, natamani mpenzi

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva nchini Marianne Mdee, ‘Mimi Mars’amesema kuwa ameshawahi kukata tamaa kwenye mahusiano baada ya kuvunjika kwa mahusiano kadhaa, ‘Break Up’.

Akihojiwa na moja ya chombo cha habari, Mimi Mars amesema kuwa hakuna kitu kibaya kama upweke unapokuwa mwenyewe unakosa raha na furaha hivyo kitu muhimu ni kuwa na mahusiano.

“Kuna kipindi unaachwa unasema mahusiano mwisho lakini hakuna kitu kibaya kama upweke ukiwa mpweke unakosa furaha na amani, lakini Mungu anakujalia unaingia tena kwenye mahusiano yananoga zaidi ya yaliopita, maisha yanaendelea,” amesema Mimi Mars.

Pia, ameongeza kuwa kwake hana muda maalumu wa kusubiri kuingia kwenye mahusiano anapoachwa au kuacha anapopata mtu mwingine basi anaingia kwenye mahusiano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live