Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mimi Jay Z na Tsh bilioni 1.2 nitachagua pesa

Jay Z Amtaka Shabiki Achukue Bil. 1 Badala Ya Kula Naye Chakula Mimi Jay Z na Tsh bilioni 1.2 nitachagua pesa

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mjadala kuwa mrefu mtandaoni watu wakilinganisha Bilioni 1.2 (kwa pesa ya Tanzania) na kupata mlo wa jioni na Jay Z, kila mtu kuchagua upande wake hatimaye mahojiano ya Jay Z na kituo cha luninga cha CBS kikahitimisha mjadala huu.

Kwenye mahojiano yake na Gayle King, hakuacha kumuuliza swali ambalo wengi walikuwa wanabishania mtandaoni ''Kati ya Tsh Bilioni 1.2 au mlo wa jioni pamoja na Jay Z) na alipoulizwa kuhusiana na swali hilo JayZ, hakuwa na kigugumizi kwenye kulijibu hilo kwa kusema mimi mwenyewe ningechagua pesa.

Gayle King: Kati ya Bilioni 1.2 (kwa pesa ya ki-Kitanzania au mlo wa jioni pamoja na Jay Z) ungechagua nini?

Jay Z: Ningechukua pesa,

Gayle King: Watu wanachagua kupata mlo na Jay Z kwa sababu wanahisi wanaweza kupata mawazo ambayo yakawa muhimu sana kwao

Jay Z: Jay Z tunaye kwenye muziki kwa muda sasa, siwezi kukwambia uchague chaguo baya chukua zako Tsh Bil 1.2 hiyo, jinunulie zako album za Jay Z sikiliza kwa sababu kila kitu kipo ndani ya muziki, kila nilichokihitaji nimekifikia na kila nilichosema nitakifanya nilikifanya pia, Kuna album ya ''The Blueprint'' ambayo kwangu mimi inaelezea maisha yangu na safari yangu kwa ujumla.

Kwa mtazamo tu Jay Z kamaliza mjadala kwa ubingwa kwa kuonesha pesa ina nguvu zaidi ya watu wanavyofikiria kiasi cha yeye mwenyewe kuchagua pesa badala yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live