Sati ni mila ya kale sana, ilikuwepo miaka mingi kabla ya hizi dini zetu za sasa, pale mume wa kihindu anapokufa basi mkewe anatakiwa kwa hiyari yake mwenyewe ajitose kwenye moto ili afe kwa ajili ya kulinda heshima ya mumewe.
Madhumuni ya mila hiyo ni kuwa wahindu wanaamini kwamba wajane hawana nafasi tena hapa duniani baada tu ya waume zao kufariki hivyo kwa heshima ya mumewe ni lazima mjane ajitose kwenye moto ili afe kishujaa.
Sio tu jamii ya Sati fahamu kuwa hata huko Katika visiwa vilivyopo kusini mwa bahari ya Pacific pia nazungumzia visiwa vya Fiji nao huwa na utaratibu kama wa kihindu endapo mtu akifariki basi ndugu wa karibu ananyongwa ili marehemu asizikwe peke yake.
Wanaamini kwamba marehemu ni lazima apate msindikizaji.