Huku akiwasaidia wafuasi na mashabiki wake, aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko amefichua kiasi cha pesa alicho nacho katika akaunti yake ya Mpesa. Ufichuzi huo umewaacha watu wengi wakizungumza huku wakionekana kushindwa kunyamaza kwani wamekuwa wakibabaishwa na fedha alizonazo.
Alikuwa na kipindi cha Live kwenye Facebook ambapo aliweka wazi nambari yake na kuwataka mashabiki kumwambia shida zinazowakabili ili ajaribu kuwasaidia.
Watu wengi walipiga simu huku wengine wakituma ujumbe wa moja kwa moja wakitafuta usaidizi. Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina Lavender alimwomba gavana huyo wa zamani amsaidie pesa za kumnunulia mtoto wake dawa. Gavana aliamua kumsaidia na kumtumia Tsh. 20000.
Baada ya hapo alishare ujumbe wa uthibitisho kuonesha ni kweli amemtumia pesa hizo na ndipo salio kwenye akaunti yake ilipofichuka. Salio lake la Mpesa lilifikia Tsh. 5259436.28. Jumla ya matumizi yake kwa mwezi huu pia yalikuwa zaidi ya Tsh. Milioni 70
Mashabiki hawakuweza kukaa kimya baada ya kupokea msaada wa Gavana huyo wa zamani wa Nairobi.