Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikasa ya Killer Mike kabla na baada ya Tuzo za Grammy

Killer Mike Grammy Mikasa ya Killer Mike kabla na baada ya Tuzo za Grammy

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Killer Mike jana alikuwa gumzo kwenye mitandao na vijiwe vyote vya mijadala ya Hip Hop duniani, ni baada ya kushinda Tuzo 3 za Grammy’s kwenye usiku ambao utabaki Kumbukumbu katika maisha yake.

Kumbukumbu hizo pia zinaletwa na mikasa ambayo imemkuta kabla na baada ya usiku wa Tuzo za Grammy’s ambapo kwa mujibu wa taarifa, Killer Mike au Jina Kamili Michael Render alikamatwa na kutiwa nguvuni na polisi wa Los Angeles kufuatia kupigana na mtu mmoja ndani ya ukumbi wa Crypto.com zilipofanyika Tuzo hizo za 66.

Video zilionesha polisi wakiwa wamemtia pingu Killer Mike huku wakielekea naye kituoni, alifunguliwa mashtaka madogo na baadaye aliachiwa kwa dhamana isiyo na malipo. Sasa muda mfupi kabla ya kukutwa na msala huo, Killer Mike (48) tayari alikuwa ametangazwa mshindi wa vipengele vyote vitatu ambavyo alikuwa nominated; Best Rap Song, Best Rap Performance na Best Rap Album (Michael)

Killer Mike amewaangusha wakali wa dunia na vipenzi vya watu akiwemo Drake, Kendrick Lamar na Nicki Minaj kwenye vipengele hivyo ikiwa ni ushindi wake wa kwanza kubeba Grammy’s katika kipindi cha zaidi ya miaka 20.

Mkasa wa pili ambao umemtokea Killer Mike baada ya usiku wa Grammy’s kumalizika ni hili tukio la mtoto wake wa Kiume kupandikizwa figo leo baada ya kusubiri kwa miaka mitatu, ili apatikane mtu wa kuendana naye. Umeripoti mtandao wa TMZ.

Novemba 2023, Killer Mike aliwahi kukaririwa akisema, anafanya sana maombi ili mtoto wake apate nafasi ya kuishi ambapo kijana huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live