Paaris, Ufaransa
Mnamo 2020, Meya Anne Hidalgo alichaguliwa tena kushika wadhifa huo kutokana na kile alichobuni kinachoitwa "mji wa dakika 15": dhana mpya ya kupanga mji ambayo inaruhusu wakazi kufanya kazi zao zote za kila siku - kuanzia manunuzi, shule hadi kazini - ndani ya dakika 15 kwa kutembea kwa miguu au kwa baiskeli.
Bogotá, Colombia
Wakati mji wa Bogota nchini Colombia kwa ujumla umekuwa na utamaduni mkubwa tu matumizi ya baiskeli, Mwaka wa 2020, Meya Claudia Lopez aliiongeza njia za ziada za kilomita 84 kwa ajili ya baiskeli. Mtandao huo wa barabara za Baiskeli ni moja mitandao mikubwa zaidi ulimwenguni.
Milan, Italia
Katika msimu wa joto wa 2020, Milan ilianza mpango kabambe wa kupanua njia za baiskeli.
San Francisco, Marekani
Jiji hili la kaskazini mwa California lilichukua hatua ya haraka wakati wa janga la Corona, kwa kuzindua kile kinachoitwa 'Mitaa ya Polepole...mpango ambao ulitumia alama na vizuizi kupunguza mwendo na misongamano ya magari na kasi kwenye njia karibu 30 katika juhudi za kuzifanya ziwe rafiki zaidi kwa watembea kwa miguu na baiskeli.