Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mihogo Festival yakusanya wasanii kibao

Mihogo ED Mihogo Festival yakusanya wasanii kibao

Mon, 19 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Baadhi ya waimbaji hao ni Mwinjuma Muumin (dansi), Nay wa Mitego (bongofleva), MC Kinata (singeli) na Safina (taarab), ambao walipagawisha mashabiki waliofika kushuhudia onyesho hilo.

Akizungumzia tamasha hilo, mratibu wake Reuben Ndege, alisema lililenga kuhamasisha vijana katika biashara ya mhongo, kuanzia kulima na kuuza ndani na hata nje ya nchi kwa vile zao hilo kwa sasa lina soko.

"Tumekuwa tukitumia wasanii mchnganyiko katika matamasha, kwa kuwa wana mashabiki wao wakiwamo wafanyabishara kama hawa waliopo Coco Beach ambao wanafanya biashara ya kukaanga mihogo," alisema.

Alisema, kwa muda mrefu wamekuwa wakizunguka ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam wakihamasisha vijana, kinamama katika kujishughulisha na kwa ajili ya kujiletea maendeleo, wakitumia kaulimbiu ya 'Mchongo mzima.

Kwa upande wake mwimbaji Mwinjuma Muumin, alisema yeye ni miongoni mwa waimbaji wa muziki wa dansi ambao wamekuwa wakishiriki matamasha hayo likiwa ni la kilele cha maadhimisho ya vibonzo duniani.

"Maadhimisho hayo yalifanyika mwezi uliopita kule Buza, nilitumia nafasi hiyo kutambulisha wimbo wangu wa 'Kwa Mpangarange Sihami', na ninaendelea kutambulisha zaidi kadri inavyowezekana," alisema Muumin.

Mkongwe huyo wa muziki wa dansi alisema, hatua ya kuitwa kwenye matamasha hayo inaonyesha wazi kuwa bado anakubalika ingawa baadhii ya watu wamekuwa wakidhani kuwa amechoka.

Alifafanua kuwa, kwa sasa ana nyimbo mpya sita za albamu ya kwanza akiwa na bendi yake ya Special Band ambayo alisema huenda ikazinduliwa rasmi Desemba mwaka huu iwapo mipango yao itakwenda kama walivyopanga.

Chanzo: ippmedia.com