Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Miezi sita jela kwa wale watakaofyatua fataki kwenye sikukuu

Miezi Sita Jela Kwa Wale Watakaofyatua Fataki Kwenye Sikukuu Miezi sita jela kwa wale watakaofyatua fataki kwenye sikukuu

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: BBC

Watu ambao watafyatua fataki huko Delhi wakati wa sikukuu za Diwali watafungwa jela hadi miezi sita, waziri wa mazingira wa jiji hilo ametangaza huku kukiwa na hali mbaya ya uchafuzi wa mazingira katika mji mkuu wa India.

Serikali ya India itatoza faini ya rupia 200 za India ($2.41; £2.15) kwa wale watakaokamatwa wakifyatua fataki.

Sheria hizo ni sehemu ya marufuku kubwa zaidi kutangazwa mnamo Septemba ili kusaidia kuzuia uchafuzi wa mazingira uliokithiri.

Delhi ndio mji mkuu uliochafuliwa zaidi ulimwenguni.

Hata hivyo sababu mbalimbali kama vile uzalishaji wa hewa kutoka kiwandani, moshi wa barabarani, na mifumo ya hewa huchangia viwango vya juu vya uchafuzi wa mazingira jijini.

Hewa huwa na sumu hasa kila msimu wa baridi wakati wakulima katika majimbo ya jirani wakichoma masalio ya mimea.

Na fataki wakati wa tamasha la Kihindi la Diwali huzidisha ubora wa hewa kwani kasi ya chini ya upepo hunasa vichafuzi katika angahewa ya chini.

Hewa iliyojaa moshi, ambayo inafunika jiji wakati huu, ina viwango vya juu vya hatari vya chembechembe ndogo zinazoitwa PM2.5 - chembe ndogo ambazo zinaweza kuziba mapafu na kusababisha magonjwa mengi.

Mwaka huu pia, ubora wa hewa unatarajiwa kuingia katika kitengo cha "kibaya zaidi" kabla ya tamasha mnamo Oktoba 24, kutokana na upepo wa utulivu na hali ya anga.

Chanzo: BBC