Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miezi sita baada ya kufariki, Lokassa ya Mbongo bado hajazikwa

Lokassa Ya Mbongo Lokassa ya Mbongo enzi za uhai wake.

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mcharaza gitaa maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Denis Lokassa Kasiya, maarufu kama Lokassa ya Mbongo, aliyefariki miezi sita iliyopita, bado mwili wake haujazikwa.

Hii imesababisha kuzuka kwa sintofahamu na wasiwasi mkubwa miongoni mwa mashabiki wake nchini mwake, barani Afrika, Ulaya na Amerika.

Lokassa 80, ambaye alifariki katika Hospitali ya St Joseph, Nashua, nchini Marekani, Machi 14, mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mrefu, alikuwa kiongozi wa bendi maarufu ya Soukous Stars, iliyokuwa na makao yake mjini Paris.

Hapo awali, aliwahi kutamba na bendi ya Tabu Ley Rochereau ya Afrisa International na baadaye bendi ya All African Stars.

Kabla mauti haijamfika, alikuwa akipambana na ugonjwa wa kisukari na kwama pia alikuwa akipata nafuu kutokana na kiharusi kidogo alichopata miaka michache iliyopita.

Mtandao wa Taifa Leo umeripoti kuwa mwili wa mwanamuziki huyo ulirudishwa nyumbani Kinshasa, ambao ni mji mkuu wa DRC, mnamo Aprili, na kwamba tangu wakati huo, mwili huo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika moja ya hospital jijini Kinshasa.

Baada ya kuwasili, mwili huo ulipokelewa uwanja wa ndege wa kimataifa wa N'Djili na wanamuziki wenzake, familia, ndugu, mashabiki na viongozi wa Serikali.

Viongozi wa muungano wa wanamuziki wa Congo, Blaise Bula na Adios Alemba waliwaongoza waombolezaji kuupokea mwili wa mwanamuziki mwenzao.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na kituo kimoja cha televisheni nchini humo, watoto wawili wa Lokassa walitoa wito kwa Serikali ya DRC, kusaidia katika mipango ya maziko ya baba yao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kinshasa, ilitarajiwa kuwa Wizara ya Utamaduni na Sanaa ingekuwa mstari wa mbele katika mipango hiyo kama ilivyokuwa kwa magwiji wengine wa muziki wa DRC.

Akizungumza na Taifa Leo hivi majuzi, mwanamuziki wa Kinshasa, Lofombe Gode amesema bado haijafahamika iwapo familia yake au maofisa wa Serikali wanafanya mipango yoyote ya maziko.

“Bado hakuna taarifa rasmi si tu kutoka kwa Serikali, bali hata kwa familia yake, zinazhusi maziko yake, maana sisi wote tunasubiri kutangazwa kwa tarehe inayotarajiwa,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live